Vyama vya Ushirika na Wakulima
Wakulima walianzisha vyama vya ushirika ili kudai bei nzuri ya mazao, kupata masoko na kupinga unyonyaji. Mifano muhimu ni:
- Bukoba Buhaya Union (1924)
- Kilimanjaro Native Planters Association (1925)
- Meru Citizens' Union (1930)
- Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU)
Mfano: KNCU iliunganisha wakulima wa kahawa katika mlima Kilimanjaro. Vyama hivi vilitoa viongozi kama Paul Bomani na Clement George Kahama ambao baadaye wakawa viongozi wa TANU.
Vyama vya Wafanyakazi
Wafanyakazi wa viwanda, bandari na mashamba walianzisha vyama kudai mishahara ya haki na mazingira mazuri ya kazi. Mifano ni:
- Tanganyika Territory Civil Servants' Association (TTCSA, 1922)
- Railway African Civil Service Union (1920)
- Tanganyika Federation of Labour (1955)
Kwa upande wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume aliunda Jumuiya ya Mabahara (1939) kwa ajili ya wafanyakazi wa vyombo vya baharini.
Vyama vya Kijamii na Kidini
Tanganyika African Association (TAA) iliundwa mwaka 1929 mjini Dar es Salaam na watumishi wa serikali. Baadaye, TAA ikazalisha chama cha TANU mwaka 1954.
Vikundi vya kidini vilichangia pia:
- Al-Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (1933) — viongozi kama Ally Sykes na Bibi Titi Mohamed
- Jamiyatu Shubbaniu Muslimin huko Zanzibar (1935)
Vilabu vya Mpira wa Miguu
Vilabu vya mpira vya Waafrika viliunganisha watu na kueneza fikra za ukombozi. Mfano ni Young African Sports Club (1935) iliyokuwa msingi wa TAA.
Vyombo vya Habari
Waafrika walianzisha vyombo vya habari vyao kwa sababu vyombo vya kikoloni havikutoa habari za harakati za kudai uhuru. Mifano ni:
- Gazeti la Kwetu (1937) — kwa African Association
- Sauti ya TANU (1957) — lililohaririwa na Mwalimu Julius Kyerere
- Sauti ya Zanzibar (1949)
Vyama vya Sanaa
Vikundi vya taarabu na lelemama vilitumika kuhamasisha wananchi. Bibi Titi Mohamed na Bibi Hawa binti Maftah waliongoza vikundi hivi. Wakati serikali ya kikoloni ilipiga marufuku mikutano, TANU iliandaa hafla za taarabu ambako Mwalimu Nyerere alikuwa akikaribishwa na kuzungumza kuhusu uhuru.
Vyama vya Sasa
Kwa Tanganyika:
- TANU (Tanganyika African National Union) — iliundwa 1954
- United Tanganyika Party (UTP) — 1956
- African National Congress (ANC) — 1958
Kwa Zanzibar:
- Zanzibar Nationalist Party (ZNP) — 1955
- Afro-Shirazi Party (ASP) — 1957
- Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP) — 1959
TANU ilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa 1960, na uhuru wa Tanganyika ulipatikana Desemba 9, 1961. Kwa Zanzibar, Mapinduzi ya Januari 12, 1964 yalileta uhuru.