Watanzania walianonesha uzalendo na ujasiri mkubwa wakati wa ukoloni kwa namna mbalimbali:
1. Mtwa Mkwawa wa Wahehe
Alizaliwa mwaka 1855 na kufariki mwaka 1898. Alikuwa kiongozi shupavu wa Wahehe huko Iringa. Mkwawa alionyesha ujasiri wake pale alipopigana na Wajerumani na kuwaua kamanda Emil von Zelewski katika vita vya Lugalo mwaka 1891. Mwaka 1894, Wajerumani waliteka ngome yake ya Kalenga, lakini Mkwawa hakukubali kuitambua serikali ya Wajerumani. Aliendelea kupigana hadi mwaka 1898, alipojipiga risasi kichwani ili asikamatwe na Wajerumani. Mkwawa alikufa kwa ajili ya uhuru wa jamii yake — hii ni mfano wa uzalendo wa hali ya juu.
2. Mangi Meli wa Old Moshi
Alizaliwa mwaka 1866 na kufariki mwaka 1900. Alikuwa kiongozi wa Wachaga huko Kilimanjaro. Mangi Meli alipigana na Wajerumani mwaka 1892 na kuwashinda, akimuua kamanda Von Bulow. Alikuwa mzalendo kwa kuwapinga Wajerumani na kufanya utawala wao kuwa mgumu. Mangi Meli alinyongwa na Wajerumani mwezi Machi mwaka 1900.
3. Kinjekitile Ngwale wa Umatumbi
Alikuwa mtaalamu wa tiba za jadi aliyeishi huko Kilwa. Mwaka 1905, aliongoza vita vya Maji Maji dhidi ya Wajerumani. Aliwaaminisha wafuasi wake kuwa risasi za wakoloni zingegcuka kuwa maji. Ingawa alikamatwa na kunyongwa mwaka 1905, alianzisha harakati ambayo iliendelea mpaka 1907 na kushawishi jamii nyingi kusimama dhidi ya ukoloni.
4. Liti Kidanka wa Unyaturu
Mwanamke huyu alizaliwa Singida alipokea ujasiri mkubwa mwaka 1903. Alipinga vitendo viovu vya wakoloni wa Kijerumani waliozora ng'ombe, mtama, na kuwakamata watu kwa kazi za lazima. Liti alitumia mbinu ya nyuki kuwaangusha askari wa Kijerumani. Alipambana hadi mwaka 1907 aliposalitiwa na kukamatwa na kunyongwa.