Chimbuko la Fasihi Andishi
Kabla ya kuwepo kwa fasihi andishi, wenyeji wa Afrika Mashariki walikuwa wana fasihi yao ya simulizi. Fasihi hii ilijumuisha:
- Hadithi: Ngano, tarihi, visasili, vigano, na soga
- Semi: Methali, misemo, mizungu, mafumbo, na vitendawili
- Ushairi simulizi: Nyimbo, mashairi, ngonjera, maghani, na tenzi
- Sanaa za maonesho: Majigambo, miviga, vichekesho, maigizo, na michezo ya watoto
Mchango Maalum wa Fasihi Simulizi
1. Tenzi kama Msingi wa Ushairi Andishi
Tenzi za zamani kama Utendi wa Fumo Liyongo zilisimuliwa kwa midomo kabla ya kuwekwa katika maandishi. Tenzi hizi zilitokana na nyimbo ambazo ndizo fasihi ya awali. Kwa mfano:
Niwezeze kwa utungo,
Hadithi yake Liyongo,
Niwezeze na mazingo,
Mambo yalomzingiya.
Beti hizi zinaakisi kipindi cha miaka ya 900-1500 BK, na lugha iliyotumika ni ile inayoakisi kipindi hicho.
2. Ngano na Hekaya kama Msingi wa Hadithi Fupi
Ngano na hekaya zilivyotafsiriwa na kuandikwa, zikawa msingi wa hadithi za awali za Kiswahili. Mifano muhimu ni:
- Swahili Tales as Told by the Natives of Zanzibar (1870) zilizotafsiriwa na Edward Steere
- Hekaya za Abunuwasi (1928)
- Alfu Lela Uleia (1928)
Visa hivi vilikuwa za kimapokeo na zenye kuingiliana na fasihi simulizi.
3. Mifano ya Riwaya Zilizochukua Umbo la Ngano na Hekaya
Kuanzia miaka ya 1940 hadi 1960, riwaya nyingi za Kiswahili zilifuata mkondo wa hekaya na ngano. Mifano ni:
- Adili na Nduguze (Robert, 1952) – ina sifa za kifasihi simulizi kama matumizi ya dialogia na balagha
- Kusadikika (Robert, 1991) – inaweza kuwa istiara kuhusu utawala wa mabavu wa kikoloni
- Kufikirika (Robert, 1968)