1. Uchambuzi wa kazi za fasihi
TEHAMA inasaidia kuchambua kazi za fasihi simulizi na andishi kwa kutumia programu mbalimbali kama vile zana za akili unde. Hii humwezesha mwandishi kuelewa vipengele vya kifasihi kama vile taswira, dhamira, na muundo wa kazi.
2. Uhifadhi na usambazaji wa kazi
Kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, WhatsApp, na YouTube, waandishi wanaweza kuhifadhi na kusambaza kazi zao kwa urahisi na haraka. Hadhira kubwa sasa inasoma kazi za fasihi mitandaoni, hivyo kukuza umakini wa wasomaji.
3. Kukuza hali za kiuchumi
Waandishi wanaweza kuweka kazi zao mitandaoni na kuzilipia wasomaji kabla ya kuzipakua au kuzisikiliza. Mfano, mwandishi anaweza kufungua jukwaa la mtandaoni na kuuza vitabu vya kazi zake, hivyo kujipatia kipato kutoka mauzo.
4. Kukuza usomaji
TEHAMA imerahisisha usomaji wa kazi za fasihi kwa kutoa vyanzo mbalimbali vya mtandaoni. Wasomaji wanaweza kusoma au kusikiliza kazi wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu au kompyuta.
5. Mawasiliano kwa waandishi
Majukwaa ya WhatsApp na makundi ya mitandao ya kijamii yamewezesha waandishi kushirikiana katika uandishi na usambazaji wa kazi zao. Waandishi wanaweza kujadili mada, kubadili mawazo, na kusaidiana katika kuboresha kazi zao.