Mbuyeku Limited ni kampuni inayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi kama vile mabati, simenti, nondo n.k. Kampuni inatoa nafasi mbili za kazi:
Mhasibu na Katibu Muhtasi
MHASIBU
Majukumu ya mhasibu ni kusimamia mahesabu ya kampuni, kuandaa ripoti za fedha, kufuatilia masuala ya kodi na kubuni mikakati ya kutumia vizuri rasilimali za kampuni.
ELIMU NA UZOEFU
- Shahada ya ACCA au CPA na Hali ya uthibitisho ya NBAA
- Ujuzi wa kanuni mbalimbali na sheria zinazohusiana na taaluma ya uhasibu
- Ujuzi wa kutumia kompyuta ya kiuhasibu
- Uzoefu wa miaka mitatu katika kusimamia mifumo ya uhasibu
- Uandaaji wa ripoti za uhasibu mahali pa kazi na shughuli nyingine za kitaaluma
KATIBU MUHTASI
Mwombaji anatarajiwa kuisaidia menejimenti katika shughuli mbalimbali za utawala na uendeshaji wa kampuni ikiwemo kupokea na kusambaza taarifa, kushughulikia barua zinazoingia na kutoka, kuandaa mikutano, kuweka mafaili katika mifumo na shughuli zingine za kiutawala.
ELIMU NA UZOEFU
- Mafunzo ya usekretari kutoka chuo kinachotambulika
- Ujuzi wa matumizi ya kompyuta
- Ujuzi wa kanuni na uelewa wa kuendesha ofisi
- Ujuzi na uzoefu wa mawasiliano na uandishi wa ripoti
- Uzoefu wa kazi ya usekretari wa miaka miwili
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji waandike barua za maombi, waambatanishe na wasifu binafsi (CV) na nakala za vyeti, namba za simu na anwani za barua pepe. Barua za maombi zinaweza kupelekwa jengo la Josam Mwenge, ofisi za Mbuyeku Limited au kutumwa kwa Meneja Mbuyeku Limited, S.L.P 2502, Dar es Salaam. Tarehe ya mwisho kupokea maombi ni tarehe 15.4.2020.
Watakaojibiwa ni wale tu watakaoorodheshwa kwa ajili ya kusailiwa