Wanywaji wa pombe hawawezi kuelezea utamu wake ulivyo. Wao hunywa tu na kufurahia ulevi wanaoupata japokuwa wapo wanaosema pombe huongeza maji mwilini, lakini hilo mimi silielewi, maji gani yanalewesha?
Wengine hudai kuwa pombe huondoa mawazo na kumfanya mtu kusahau matatizo yake, hili nalo nalichakachua kichwani naona ni uongo kwa vile pombe huzidisha matatizo. Ikiisha mwilini hali liubaki kuwa kama mwanzo.
Hata hivyo, bado ninaamini kuwa pombe inamadhara mengi kuliko faida. Pombe inamaliza pesa, humfanya mtu kuwa mzembe, husababisha ajali, wengi huwa hawajali usafi, hawajali Watoto wao, chakula chao, mavazi na gharama nyingine. Mimi ninaamini kuwa tusipoendekeza pombe tutapiga hatua kubwa katika maendeleo yetu, yajamii na Taifa kwa ujumla.